Jambazi latoroka chini ya ulinzi
Thursday, 21 April 2011 10:42
- Ni saa chache baada ya kukamatwa
- Mengine mawili yauawa kwa risasi
- Wananchi waua polisi kwa mapanga
polisi akiweka sawa bastola
Na Peter Katulanda, Mwanza
MTUHUMIWA sugu wa ujambazi maarufu kama Askofu, ametoroka akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi. Askofu ni miongoni mwa majambazi manne yaliyotiwa mbaroni juzi jioni, eneo la Libert mjini hapa wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu, ambapo wenzake watatu wameuawa kwa kutwangwa risasi.
Jambazi hilo , linatajwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhalifu, ambapo miezi miwili iliyopita alichiwa huru na mahakama kutokana na kukoseka kwa ushahidi wa kumtia hatiani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, alisema jana Askofu na wenzake walijaribu kutoroka wakati Polisi wakifukua bunduki aina ya SMG, ambayo waliificha ardhini.
“Walikiri kumiliki SMG kinyume cha sheria na kuitumia katika uhalifu. Walikubali kwenda kuonyesha silaha hiyo na wakati polisi wakifukua, yalijaribu kutoroka na askari wakalazimika kuwafyatulia risasi,” alisema.
CHADEMA: Tutahoji utajiri wa Ridhiwan
Thursday, 21 April 2011 08:17
Na Geofrey Nyang'oro, Singida
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willbroad Slaa amesema chama chake kinajipanga kuhoji kile alichodai utajiri mkubwa wa ghafla wa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji na pia Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Dk Slaa alisema hayo jana katika Kijiji cha Ikungi, mkoani Singida alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara. Alisema anajua kuwa mjumbe huyo (jina tunalihifadhi kwa kuwa jitihada za kumpata kujibu tuhuma hizo hazikufanikiwa), licha ya umri wake mdogo hivi sasa ana fedha nyingi. Katika mkutano huo Dk Slaa alimtuhumu kuwa na utajiri uliopindukia ambao alisema haulingani na umri wake.
…. Kwa habari zaidi, ingia kwenye hii source:
Zitto ‘amgeuzia kibao’ CAG
Thursday, 21 April 2011 08:56
Ruzuku vyama vya siasa
- Adai ameshindwa kukagua Sh83 Bilioni
Mh. Zitto Kabwe
Na Kizitto Noya
WAZIRI Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe ametaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ichunguzwe kwa uzembe wa kushindwa kukagua hesabu za ruzuku za vyama vya siasa kwa muda wa miaka mitatu.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kabwe alisema CAG ameshindwa kukagua ruzuku ya Sh83 bilioni iliyotolewa kwa vyama vya siasa nchini tangu mwaka 2005 hadi 2010. Alisema ingawa kuna tatizo katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, CAG hawezi kumtupia mzigo huo pekee yake kwani naye anahusika.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kabwe alisema CAG ameshindwa kukagua ruzuku ya Sh83 bilioni iliyotolewa kwa vyama vya siasa nchini tangu mwaka 2005 hadi 2010. Alisema ingawa kuna tatizo katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, CAG hawezi kumtupia mzigo huo pekee yake kwani naye anahusika.
…. Kwa habari zaidi, ingia kwenye hii source:
Dk. Slaa afichua mabilioni ya Rostam
• Asema anapokea bil. 280/- kwa mwaka, ataka akamatwe
Dk. Willibrod Slaa
Na Joseph Senga
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mapato ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kwa kile alichodai yana uhusiano mkubwa na ufisadi.
Dk. Slaa aliyasema hayo juzi jioni katika mkutano wake mjini Igunga, mkoani Tabora katika mwendelezo wa ziara zake.
Alisema mapato ya Rostam kwa mwaka yanafikia sh bilioni 280, hivyo TAKUKURU haina budi kumkamata na kumchunguza kwani aliwahi kutangaza kuwa hana shida ya kuwa kiongozi au kung’ang’ania madaraka yoyote, kwani pesa alizonazo zinamtosha.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa TAKUKURU haitamchukulia hatua Rostam, atawashawishi wananchi kutotoa ushirikiano wowote kwa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwazomea maofisa wake kila wanapowaona. Akifafanua tuhuma hizo za ufisadi, alisema kuwa kati ya makampuni 17 yanayosemekana kuwa ni ya Rostam hakuna jina lake hata moja.
…. Kwa habari zaidi, ingia kwenye hii source:

No comments:
Post a Comment