Friday, April 22, 2011

BREAKING NEWS!

Kikwete abariki nyongeza ya mishahara
Friday, 22 April 2011 09:41

    *asema hatabinafsisha tena TRL, Bandari

RAIS Jakaya Kikwete  

Patricia Kimelemeta  RAIS Jakaya Kikwete ameahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi kupitia bajeti ya Serikali katika mwaka wa fedha, 2011/2012. Rais Kikweta alitoa ahadi hiyo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Ikulu jijini Dar es Salaam. Mkutano baina ya Tucta na Rais ni wa kwanza tangu Kikwete achaguliwe kwa mara ya pili kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana.

Katika mwaka wake wa mwisho wa ngwe ya kwanza ya uongozi wake, Serikali ya Kikwete iliingia katika malumbano makali kuhusu suala la stahili za wafanyakazi na mishahara midogo iisiyolingana na gharama za maisha.

Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalumu jana kuwa, pamoja na mambo mengine, Rais ameahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi ili kuwapunguzia makali ya maisha.  “Mishahara ya wafanyakazi ni midogo, ikilinganishwa na kipindi hiki cha kupanda kwa gharama za maisha. Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete ameihaidi kuongeza mishahara kwenye bajeti hii ya fedha ya mwaka 2011/12,”alisema Mgaya.
..... kwa taarifa zaidi, ingia kwenye hii source:

Nape aonya hakuna fisadi atakayepona

Thursday, 21 April 2011 19:12 newsroom
  • Asisitiza agizo la siku 90 lipo palepale
  • Mr Nape Nnauye
CHAMA Cha Mapinduzi kimesema hakitarudi nyuma wala kukata tamaa katika mkakati wake wa kuwaondoa watuhumiwa wa ufisadi ambao wamepewa miezi mitatu kujitafakari na kujiengua wenyewe. Kimesisitiza kwamba watuhumiwa ambao hawataki kuachia nyadhifa zao kwa hiari, wataondolewa kwa nguvu ya Chama, licha ya kuwatumia baadhi ya wanasiasa, vyombo vya habari na viongozi wa dini kuwachafua viongozi waandamizi wa Chama na kupotosha ukweli.

Kauli hiyo ya CCM imekuja baada ya baadhi vyombo vya habari kuanza kuandika habari za kuwadhoofisha viongozi wa Sekretarieti mpya ya CCM kwa lengo la kupunguza kasi ya utekelezaji wa mikakati ya kuwaondoa watu hao katika nafasi za uongozi. Akizungumza na Uhuru jana, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kila wanachokisema kwenye mikutano ya kujitambulisha ni maamuzi yaliyopitishwa kwenye vikao vya Chama na si msimamo wa mtu mmoja.

..... kwa taarifa zaidi, ingia kwenye hii source:



 Makinda atakiwa kulinda heshima ya Bunge
21st April 2011 @ 23:59
 Anne Makinda

Na Stella Nyemenohi
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema Spika wa Bunge anapaswa kutumia wadhifa wake na kanuni za Bunge kulinda heshima ya Bunge. LHRC imeainisha kasoro zilizojitokeza katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 10 uliomalizika Dodoma Aprili 16. Kituo hicho kimesema kulikuwa na ukiukwaji wa maadili na kanuni za Bunge, kwa baadhi ya wabunge na kusema umefika wakati, Spika atumie mamlaka na kanuni zilizopo, ili wabunge waache kutumia lugha zisizo na staha bungeni.

“Spika atumie mamlaka na kanuni za Bunge ili kudhibiti maudhui, mantiki na maana ya mijadala ya Bunge bila kuathiri maslahi ya taifa … Spika ana dhamana ya kuhakikisha ushabiki wa kisiasa haupati nafasi kuvuruga Bunge,” amesema Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urio.






..... kwa taarifa zaidi, ingia kwenye hii source:

Thursday, April 21, 2011

NEWS! NEWS!

Jambazi latoroka chini ya ulinzi

Thursday, 21 April 2011 10:42 
  • Ni saa chache baada ya kukamatwa
  • Mengine mawili yauawa kwa risasi
  • Wananchi waua polisi kwa mapanga
polisi akiweka sawa bastola

Na Peter Katulanda, Mwanza
MTUHUMIWA sugu wa ujambazi maarufu kama Askofu, ametoroka akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi. Askofu ni miongoni mwa majambazi manne yaliyotiwa mbaroni juzi jioni, eneo la Libert mjini hapa wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu, ambapo wenzake watatu wameuawa kwa kutwangwa risasi.

Jambazi hilo, linatajwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhalifu, ambapo miezi miwili iliyopita alichiwa huru na mahakama kutokana na kukoseka kwa ushahidi wa kumtia hatiani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, alisema jana Askofu na wenzake walijaribu kutoroka wakati Polisi wakifukua bunduki aina ya SMG, ambayo waliificha ardhini.

 “Walikiri kumiliki SMG kinyume cha sheria na kuitumia katika uhalifu. Walikubali kwenda kuonyesha silaha hiyo na wakati polisi wakifukua, yalijaribu kutoroka na askari wakalazimika kuwafyatulia risasi,” alisema.

…. Kwa habari zaidi, ingia kwenye hii source:



CHADEMA: Tutahoji utajiri wa Ridhiwan
Thursday, 21 April 2011 08:17

Ridhiwani J K akiwa na waifu wake Bi. Arafa Mohamed
Na Geofrey Nyang'oro, Singida
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willbroad Slaa amesema chama chake kinajipanga kuhoji kile alichodai utajiri mkubwa wa ghafla wa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji na pia Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Dk Slaa alisema hayo jana katika Kijiji cha Ikungi, mkoani Singida alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara. Alisema anajua kuwa mjumbe huyo (jina tunalihifadhi kwa kuwa jitihada za kumpata kujibu tuhuma hizo hazikufanikiwa), licha ya umri wake mdogo hivi sasa ana fedha nyingi. Katika mkutano huo Dk Slaa alimtuhumu kuwa na utajiri uliopindukia ambao alisema haulingani na umri wake.
…. Kwa habari zaidi, ingia kwenye hii source:


Zitto ‘amgeuzia kibao’ CAG
Thursday, 21 April 2011 08:56

Ruzuku vyama vya siasa
  •  Adai ameshindwa kukagua Sh83 Bilioni

Mh. Zitto Kabwe

Na Kizitto Noya

WAZIRI Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe ametaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ichunguzwe kwa uzembe wa kushindwa kukagua hesabu za ruzuku za vyama vya siasa kwa muda wa miaka mitatu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kabwe alisema CAG ameshindwa kukagua ruzuku ya Sh83 bilioni iliyotolewa kwa vyama vya siasa nchini tangu mwaka 2005 hadi 2010. Alisema ingawa kuna tatizo katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, CAG hawezi kumtupia mzigo huo pekee yake kwani naye anahusika.

…. Kwa habari zaidi, ingia kwenye hii source:


Dk. Slaa afichua mabilioni ya Rostam

•  Asema anapokea bil. 280/- kwa mwaka, ataka akamatwe

 
Dk. Willibrod Slaa
Na Joseph Senga
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mapato ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kwa kile alichodai yana uhusiano mkubwa na ufisadi.

Dk. Slaa aliyasema hayo juzi jioni katika mkutano wake mjini Igunga, mkoani Tabora katika mwendelezo wa ziara zake.

Alisema mapato ya Rostam kwa mwaka yanafikia sh bilioni 280, hivyo TAKUKURU haina budi kumkamata na kumchunguza kwani aliwahi kutangaza kuwa hana shida ya kuwa kiongozi au kung’ang’ania madaraka yoyote, kwani pesa alizonazo zinamtosha.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa TAKUKURU haitamchukulia hatua Rostam, atawashawishi wananchi kutotoa ushirikiano wowote kwa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwazomea maofisa wake kila wanapowaona.  Akifafanua tuhuma hizo za ufisadi, alisema kuwa kati ya makampuni 17 yanayosemekana kuwa ni ya Rostam hakuna jina lake hata moja.

…. Kwa habari zaidi, ingia kwenye hii source: